home

 


Historia ya kwaya Bandeko

Kikundi hiki kilizaliwa katika Milano kutokana na mang’amuzi ya baadhi ya vijana waliokuwa wamekwenda Afrika na Amerika ya kusini kufanya kazi za kujitolea. Mpango huu ulikuwa umepangwa na kikundi cha “Africa Oggi” – Afrika Leo.

Kwenye miaka ya mwanzo ya tisini ('92/'93), kikundi cha vijana wapato kumi walikuwa wanakusanyika kwa ajili ya kuandaa na kuimba nyimbo za misa takatifu. Huu ulikuwa wakati mahususi sana wa kuwakutanisha na kuwaunganisha vijana wa “Africa Oggi”. Nyimbo hizi za lugha ya kigeni zimekuwa kama chombo cha kusaidia kuishi maisha ya kiroho, na vilevile kushirikisha waumini zaidi katika sadaka ya misa takatifu.

Siku moja, vijana wawili (wanachama wa Bandeko) walitaka kufunga ndoa yao kanisani. Hivyo basi waliwaomba kwaya ya Bandeko waimbe wakati wa misa ya ndoa yao (Monza 03/09/1993). Tangu wakati huo, kikundi cha kwaya ya Bandeko walianza kupapa mialiko katika Parokia mbalimbali kwa ajili ya kwenda kuimba wakati wa ibada za misa za kimisionari. Kwa kweli lilikuwa wazo zuri sana kuwajibika namna hii kwani ilikuwa njia mojawapo ya kukusanya sadaka/msaada wa pesa ambao ulisaidia miradi mbalimbali ya mshikamano na misioni.
Kwenye mwaka wa 1996, kwaya ilijichagulia jina la Bandeko.

Kutoka wakati huo, kwaya yetu ilizidi kujulikana sana kiasi kwamba tulianza kupata mialiko mbalimbali kama vile: sikukuu za halaiki, sherehe za ubatizo, siku za kimisionari, katika mihadhara mbalimbali na maandamano ya amani, na sherehe nyingine nyingi.
Mpaka siku hizi bado tunaendelea kujifunza nyimbo mpya. Tunafanya mazoezi ya nyimbo mpya na za zamani mara moja kwa wiki.

 

 

 

 

 

Mappa del sito