|
|
|
Mawasiliano
ya marafiki:
Afrika Leo: Ni kikundi kilichoanzishwa na Bwana Adriano
Zanini. Kuanzia mwaka 1978, chama cha Africa Oggi kimekuwa kikiandaa safari
na mipango ya kazi za kujitolea kwa ajili ya misioni za Afrika na Amerika
ya Kusini. Katika mipango yote hii wamekuwa wanashirikiana na wamisionari
mapadri na masista. Zoezi hili la kushikamana na misioni limewasaidia
sana wanachama wa Bandeko kufahamu mazingira na hali ya maisha ya nchi
za misioni, mila na desturi zao, nakadhalika.
Lengo la Bandeko ni “Kuwa wazi na kujitolea kwa ajili ya wengine”
Mradi wa Kalicero: Ni kikundi cha
watu wenye lengo la kuwajibika katika kusaidia nchi zinazoendelea, na
pia kukuza mawasiliano ya vyombo vya habari (magazeti, majalida, vitabu,
...) kwa lengo la kusaidia kutoa hali halisi ya nchi hizi. Kwa kweli shughuli
kubwa ni kuwatayarisha wataalamu wananchi katika nyanja za elimu ya afya
na majaribio/mazoezi katika kituo che utapiamlo che Kalicero. Zaidi ya
hayo, inatoa huduma za afya katika kituo cha afya cha “Muzeyi Health
Center” (Kituo cha afya cha Muzeyi).
|
|