home

 


Mpaka kuweza kufanikisha huu mtandao haikuwa kazi rasisi. Hata hivyo, hilo siyo tatizo, muhimu ni kwamba tumefanikiwa.

Wazo hili lilikuwepo tangu mwaka wa 1999 (elfu moja mia tisa na tisini na tisa): baada ya subira nyingi tulifanikiwa kusahihisha maneno/maandishi ya baadhi ya nyimbo ambazo wanakwaya wetu (wa zamani na wapya) wangependa kutushirikisha. Shukrani za dhati ziwaendee wale wanakwaya wote walioshiriki katika kusanii nyimbo hizi.

Shukrani nyingi sana zimwendee Davide na Vincenzo kwa kazi kubwa ya ufundi na ustadi aliyofanya ya kubuni huu mtandao. Asante, umefanya kazi nzuri sana. Nakushukuru hata kwa saburi nyingi uliyokuwa nayo katika kutafsiri maoni yangu. Nina imani kuwa kazi hii ya kutayarisha huu mtandao itakuletea sifa na umaarufu mwingi ndani ya Bandeko.

Shukrani nyingine ziwaendee wafuatao:
Paolo (Pauli) kwa tafsiri katika lugha ya Kihispania. Kazi yako imeboresha nakala yetu katika lugha ya Kiitaliano.
Padri Salutaris, mmisionari wa shirika la Waconsolata, kwa tafsiri katika lugha ya Kiswahili, kitu ambacho, kwa namna ya pekee nijivunia kwa sababu inatuwezesha kurusha hewani mang’amuzi yetu katika lugha ambayo imeenea sana katika bara la Afrika, ambayo kwayo wengi wetu tunaitumia. Tunawashukuru wote wawili, ninyi na ndugu zetu kabisa.

Tunatumaini kwamba, mtandao huu hautakuwa tu chombo cha kutoa ushuhuda wa mang’amuzi mbalimbali, bali utakuwa ishara ya amani na umoja kwa wale wote ambao watautembelea.

Carlo

 

 

 

 

 

Mappa del sito